Kambi ya timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), imeanza rasmi leo Oktoba Mosi kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Afrika (AFCON 2019) dhidi ya Cape Verde.
Kambi hiyo inawahusisha wachezaji wanaocheza kwenye ligi kuu ya soka Tanzania bara, na baadae wataungana na wale wanaocheza nje ya Tanzania.
Mazoezi ya Taifa Stars inayonolewa na kocha kutoka nchini Nigeria, Emmanuel Amunike kwa kusaidiana na Hemed Morocco na Emeka Amadi; Madaktari Richard Yomba na Gilbert Kigadya, yanatarajiwa kuanza kesho asubuhi kwenye Uwanja wa JMK Park, Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.
Taifa Stars itacheza mchezo wake dhidi ya Cape Verde Oktoba 12 mjini Praia, na siku nne baadaye itakua nyumbani Dar es salaam, kucheza mchezo wa marudiano kwenye Uwanja wa Taifa.
Kocha Amunike juma lililopita alitangaza kikosi cha wachezaji 30 kwa ajili ya michezo hiyo miwili ambapo upande wa walinda mlango yupo, Aishi Manula (Simba), Mohamed Abdulrahman (JKT) na Benno Kakolanya (Young Africans).
Mabeki: Shomary Kapombe (Simba), Hassan Kessy (Nkana, Zambia), Salum Kimenya (Tz Prisons), Paulo Ngalema, Ally Sonso (Lipuli) Abdi Banda (Baroka, Afrika Kusini), , Gadiel Michael, Kelvin Yondani , Andrew Vincent Dante (Young Africans) Abdallah Kheri, Agrey Morris na David Mwantika (Azam).
Viungo: Himid Mao (Pertojet, Misri), Jonas Mkude (Simba), Frank Domayo , Mudathir Yahya (Azam), Feisal Salum (Young Aficans), Saimon Msuva (El Jadidi, Morocco), Farid Mussa (CD Tenerife, Hispania), Salum Kihimbwa (Mtibwa).
Washambuliaji: Mbwana Samata (Genk, Ubelgiji), John Bocco (Simba), Thomas Ulimwengu (A Hilal, Sudani), Rashid Mandawa (BDF XI, Botswana), Yahya Zayd (Azam), Shaban Chilunda (CD Tenerife, Hispania) na Kelvin Sabato (Mtibwa Sugar).