Shirikisho la Soka nchini (TFF) limetangaza mapato ya mchezo namba 72 wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara (TPL) kati ya Simba na Young Africans, uliochezwa jana Jumapili, Septemba 30, 2018 Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na shirikisho hilo, mchezo huo uliokua unasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka nchini kote na kumalizika kwa sare ya bila kufungana, uliingiza jumla ya shilingi milioni 404,549,000.

Taarifa hiyo ya TFF imeeleza kuwa, mchezo huo ulioanza mishale ya saa 11 jioni uliingiza jumla ya Watazamaji 50,168.

Hata hivyo, TFF imeonesha mgawanyo wa mapato hayo ambao umeihusisha TRA (VAT), Selcom, TFF, Uwanja, Simba, TPLB, gharama za mchezo, BMT na DRFA.

Kati ya fedha hizo VAT ambayo ni asilimia 18 ni shilingi milioni 61,710,864.41, Selcom milioni 17,901,293.25.

Shirikisho la soka nchini TFF limepata milioni 16,246,842.12, Uwanja milioni 48,740,526.35.

Wenyeji wa mchezo Simba milioni wamepata 194,962,105.41, TPLB milioni 29,244,315.81, gharama ya mchezo 22,745,578.96, BMT milioni 3,249,368.42 na DRFA milioni 9,748,105.27.

Navy Kenzo wajiunga WCB baada ya 'Katika' na Diamond?
Taifa Stars yaanza kuiwinda Cape Verde