Takribani watu 150 wamekufa katika Wilaya ya Itaewon mjini Seoul nchini Korea Kusini, katia eneo maarufu la burudani za usiku ambalo hutembelewa zaidi na vijana au wageni, lililosheheni migahawa na sehemu za kujiburudisha kufuatia mkanyagano ulitokea wakati wa kusherekea sikuku ya Halloween.

Kufuatia tukio hilo la Oktoba 29, 2022, Rais wa nchi hiyo, Yoon Suk-yeol ameamuru maafisa kupeleka timu za huduma ya kwanza na kuweka tayari vitanda hospitalini kwa walioathirika, huku Meya wa Seoul Oh Se-hoon, ambaye alikuwa barani Ulaya, akilazimika kukatisha ziara yake.

Kwa mujibu wa maafisa wa zimamoto wa eneo hilo, wamesema watu waliendelea kumiminika kwenye uchochoro mwembamba ambao tayari ulikuwa umefurika, wakati wengine waliokuwa juu ya barabara yenye mteremko wakianguka na kuwaangusha wengine.

Wahudumu wa uokozi katika eneo la mkasa wa mkanyagano. Picha: Lee ji-eun/ AP

Afisa wa idara ya Zimamoto, Choi Seong-beom amesema “idadi kubwa ya majeruhi ilitokana na wengi kukanyagwa wakati wa sherehe za Halloween,” akiongeza kwamba idadi ya waliokufa huenda ikaongezeka.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, limesema shuhuda mmoja aliyejulikana kwa jina la Monn Ju-Young alisema “kulikuwa na dalili zote kwamba kutakuwa na tatizo kwenye uchochoro kabla ya tukio na bado watu waliendelea kufurika nila kuhofia.”

Hata hivyo, baadhi ya mashuhuda wengine wameelezea matukio ya ghasia muda mfupi kabla ya kutokea mkanyagano, huku Polisi waliokuwa wakifuatulia sherehe hizo za Halloween wakishindwa kudhibiti umati mkubwa wa watu.

EMA yatoa tahadhari chanjo ya Uviko-19

Baadhi ya mabaki ya mavazi ya Halloween. Picha: Chung Sung

Aidha, picha za mitandao ya kijamii zimeonyesha mamia ya watu wakiwa wamejazana kwenye kichochoro chembamba kilichopo kwenye mteremko, huku Polisi na maafisa wa msaada wa dharura wakijaribu kuwavuta na kuwatoa.

Picha nyingine, zimeonesha matukio ya maafisa na raia wakiwapatia huduma ya kwanza watu wengi ambao walionekana kupoteza fahamu, huku Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz akituma salamu za rambirambi kufuatia mkasa huo na kusema “ni tukio la kutisha huko Seoul na imetushtua sisi sote.”

Rais wa Marekani, Joe Biden amesema Marekani “inasimama pamoja” na Korea Kusini kufuatia mkanyagano uliosababisha vifo vya watu kwenye sherehe za Halloween katika mji mkuu wa nchi hiyo.

Ulinzi ukiwa umeimarishwa katika eneo hilo, huku wafanyakazi wa kutoa huduma wakiendelea na zoezi la uokoaji. Picha: Chung Sung/ AFP

Ukiacha kusoma unaacha kuongoza: Msigwa
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Octoba 30, 2022    Â