Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini – TAKUKURU, Mkoa wa Dodoma kwa kipindi cha miezi mitatu kuanzia Julai hadi Septemba imepokea Malalamiko 165 ambapo 53 kati ya hayo hayakuhusu rushwa na walalamikaji 30 walielimishwa, huku malalamiko 10 yakihamishiwa Jeshi la Polisi.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Mkuu wa Taasisi hiyo Mkoa wa Dodoma, John Joseph amesema malalamiko 112 yalihusu rushwa ambayo iliyopelekea kufunguliwa Majalada ya uchunguzi.

Amesema, “kati ya Majalada hayo 112 uchunguzi wa majalada 12 yamekamilika na majalada matano (5) yamewasilishwa katika ofisi ya mashtaka kwa hatua zaidi na majalada matano (5) vibali vya kufungua mashauri vimetolewa.”

Aidha, Joseph ameongeza kuwa pamoja na utekelezaji wa majukumu ya kawaida pia wamejiwekea malengo ya kutekeleza vipaumbele vinavyolenga kuzuia vitendo vya rushwa na kwamba wataendelea kufuatilia kero za migogoro ya Ardhi ambayo imekuwa ikilalamimikiwa kila kukicha.

“Tutafuatilia miradi ya ujenzi wa madarasa,vituo vya afya na miradi mingine ambayo bado inaendelea kujengwa kupitia fedha za kuimarisha elimu ya awali na Msingi, tutaongeza kasi ya ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili kuziba mianya ya rushwa na ufujaji,” amesema Joseph.

Robertinho aipa mbinu Young Africans
Jamii iongoze kutokomeza UKIMWI