Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Tanga, imeokoa Shilingi Milioni 30.5 za Chama cha Walimu cha kuweka na kukopa wilaya ya Korogwe zilizokuwa zimefanyiwa ubadhirifu na baadhi ya waliokuwa viongozi wa chama hicho.
Taarifa hiyo imetolewa kwa vyombo vya habari na Kaimu Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Tanga, Dkt. Sharifa Bangala leo Septemba 18, 2020.