Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Innocent Bashungwa amesema takwimu zitakazokusanywa kwenye Sensa ya Watu na Makazi itakayofanyika tarehe 23 Agosti,2022 zitasaidia kuimarisha upelekeaji wa huduma kwa wananchi.
Waziri Bashungwa ameyasema hayo na kudai kuwa upangaji wa mipango mbalimbali ya maendeleo hasa ya upelekaji wa huduma za kijamii na kiuchumi karibu na Wananchi zinahitaji takwimu sahihi ya idadi ya watu ili huduma hizo ziwezi kuendana na idadi ya watu.
Amesema, “Huduma kama ujenzi wa vituo vya kutolea huduma za afya na zahanati, madarasa, miundombinu ya maji na barabara maabara pamoja na mgawanyiko wa watumishi kwenye Mamlaka za Serikali.”
Bashungwa ameongeza kuwa, TAMISEMI itatekeleza upatikanaji wa huduma za afya bure kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano haziwezi kutekelezeka kwa ufanisi iwapo kutakuwa hakuna takwimu sahihi na kwamba sensa ya watu na makazi itasaidia kufanikisha zoezi hilo.