Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI imesema kuwa dawa ya waliowatelekeza watoto iko jikoni na imeowaonya wanaombeza Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda kwa zoezi alilolianzisha.

Imesema kuwa serikali inakusudia kuipa nguvu sheria inayowalinda watoto kwamba hadi juni mwaka huu marekebisho yatakuwa yamekamilika.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa TAMISEMI, Joseph  Kakunda katika mahafali ya kidato cha nne ya shule ya Seminari ya Kiislamu ya Al- Farouq Tabata jijini Dar es salaam.

“Kumlea mtoto kwasasa litakuwa ni jukumu la lazima kwa kila mzazi, ninasifu hatua zilizochukuliwa na Paul Makonda, za kushughulikia watoto waliotelekezwa,”amesema Kakunda

Amesema kuwa hata kama kuna kigogo yeyote au kiongozi wa dini aliyetelekeza mtoto ni lazima amhudumie vinginevyo sheria itachukua mkondo wake.

Hata hivyo, Kakunda ameongeza kuwa sheria itaendelea kuunga mkono sekta binafsi katika kuwekeza katika shughuli za maendeleo hususani elimu.

 

 

 

Video: Aliyegandwa na kiroba asimulia kilichomponza, Vigogo wagongana
Wasiojulikana wateketeza Mahakama ya Mwanzo