Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli leo hii Mei 5, 2018 katika ziara yake ya kikazi Mkoani Morogoro amechangia kiasi cha pesa shilingi milioni 3 kwa shule ya Sekondari Mang’ula kwa ajili ya ujenzi wa choo.

Rais Magufuli amemsimamisha mwanafunzi mmoja wa shule ya Mang’ula na kumkabidhi kiasi hiko cha pesa mara baada ya mwanafunzi huyo wa kidato cha kwanza kuwasilisha tatizo hilo la choo kwa Rais Magufuli.

Aidha Rais amewataka wazazi wa wanafunzi wa shule hiyo kuchangia kiasi kilichobaki kuhakikisha ujenzi wa choo katika shule hiyo unakamilika, amesema ujenzi ukikamilika atatembelea ili kukagua vyoo hivyo.

Bonyeza kitufe hapo chini kutaza video hiyo.

Video: JPM atoa kauli kuhusu bomoabomoa Mang'ula
Rais asema Taifa lakumbwa na msiba mkubwa