Waziri wa afya, Ummy Mwalimu amesema amefarijika kuona hospitali ya Mloganzila ambayo ipo chini ya Hospitali ya Taifa Muhimbili inatoa huduma vizuri kinyume na hisia za baadhi ya wananchi kuwa huduma za Mloganzila ni mbaya na hivyo kupelekea wagonjwa wengi kufariki.
Amekanusha uvumi wa watu ambao wanasema wanaohudumia wagonjwa ni madaktari wanafunzi kwa kusema huduma zote zinatolewa na madaktari bingwa.
“zipo hisia potofu kuwa wanaohudumia wagonjwa ni wanafunzi, Leo nikiwa pamoja na wanahabari tumejionea ukweli kuwa huduma zinatolewa na madaktari na madaktari bingwa” Amesema waziri Mwalimu
Na kuongeza “kama ilivyo Hospitali nyingine kubwa nchini mfano Muhimbili, MOI, Bugando, KCMC, Hospitali ya Mloganzila huwa pia inatumika kufundishia wanafunzi wa udaktari na fani nyingine za afya”
Amefafanua kuwa madaktari ho wanafunzi nao husaidiana na madaktari bingwa katika kuwahudumia wagonjwa, Lakini huwa wanasimamiwa na madaktari na madaktari bingwa.
Aidha amekiri uwepo wa changamoto kadhaa ambazo wameanza kuzifanyia kazi kwa lengo la kuzitatua, Changamoto hizo ni pamoja na uhaba wa watumishi, ugumu wa usafiri wa kwenda mloganzila (Manispaa ya Ubungo wanajenga kituo cha mabasi), utaratibu wa ndugu kuona wagonjwa (hospitali imejengwa ki-western kwa kuzingatia kuwa mgonjwa atatembelewa na ndugu mmoja au wawili kwa siku.
“Sasa kwa utamaduni wetu mgonjwa wetu huwa anatembelewa na watu wengi hadi ndugu 10 kwa siku, Hospitali ina lift 6 tu sasa endapo kila mgonjwa atatembelewa na ndugu 10, ina maana lift zihudumie watu kuwanzia 3,000 katika muda wa masaa mawili ya kuwaona wagonjwa hii imekuwa kero kwa ndugu kwa kuwa hutumia muda mwingi kusubiri kuona wagonjwa wao” Amebainisha Waziri Ummy.