Boniface Gideon – Tanga.

Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Tanga – Tanga UWASA, imekabidhi vyoo kwa shule za msingi na Sekondari Funguni, ikiwa ni sehemu ya mradi wanaoutekeleza Wilayani Pangani uliogawanywa katika sehemu tatu za ujenzi wa miundombinu ya kupokea na kutibu taka ngumu na uliopo mbioni kukamilika.

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira – Tanga UWASA, Mhandisi Geofrey Hilly amesema inatekelezwa kupitia ufadhili wa Serikali wa Shilingi Bilioni moja kiasi kilichothibitishwa na MJbunge wa Jimbo la Pangani na Waziri wa Maji, Jumaa Aweso.

Amesema, “tumelenga kutoa maji maji safi na salama, Tanga UWASA imetekeleza mradi huu kwa lengo la kuboresha huduma kwa wakazi wa mji wa Pangani na nje ya Pangani na umejengwa kwa ufadhili wa serikali kwa gharama ya shilingi billion moja na utakamilika Septemba 30,2023.”

Awali, akikabidhi moja ya mradi wa choo katika shule ya msingi Funguni, Mkuu wa Wilaya ya Pangani, Zainab Abdallah aliwapongeza Tanga UWASA kwa kufikisha kuduma karibu na Wananchi sambamba na kujali afya zao kwa kujenga vyoo kwenye maeneo yanayowazunguka.

Ujenzi wa mradi huo, umefikia asilimia 92 katika maeneo matatu ya shule ya msingi na sekondari Funguni na iliyokamilika ni asilimia 100 pamoja na eneo la kituo kikuu cha mabasi uliofikia asilimia 98 na ukilenga kuwakinga na magonjwa ya mlipuko wananchi wanaozunguka maeneo hayo.

Bruno Fernandes aukwaa unahodha Man Utd
Rasmi Luis Miquissone arejea Simba SC