Uingereza imepiga marufuku wasafiri wote kutoka Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), kuingia nchini humo ikiwa ni hatua za kuzuia kuenea kwa maambukizi ya Virusi vya Corona, kutokana na aina mpya ya kirusi kilichogunduliwa nchini Afrika Kusini.
Taarifa hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi wa nchi hiyo Grant Shapps, kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Twitter, na kusema kuwa zuio hilo linaanza leo Januari 22, 2021.
“Abiria wote kutoka nchi hizo isipokuwa, Uingereza na Jamhuri ya Irand na nchi za kutoka Dunia ya tatu ambao wana vibali vya ukaazi hawatoruhusiwa kuingia”, ameandika Shapps.
Aidha Shapps ameongeza kuwa, “Tunaendelea kufuatilia mwenendo wa maambukizi ya Virusi vya Corona, pamoja na aina mpya ya virusi kote Dunia pamoja na hii hatua ya kuzuia watu kusafiri na upimaji wa virusi hivyo kwa wasafiri kabla ya kuondoka itasaidi kulinda mipaka yetu”.