Mfanyabiashara Maarufu nchini, Rostam Aziz amehimiza suala la umoja wa Kitaifa akisema nchi ya Tanzania ina bahati na ni kisiwa cha amani katika eneo lenye migogoro mingi ndani ya bara la Afrika.

Rostam ameyasema hayo wakati akichangia mjadala wa sakata la Bandari na kuongeza kuwa ni lazima kuwashukuru waasisi wa Taifa hili ambao wameibeba Tanzania mpaka hii leo na hakuna mtu anayeulizwa dini yake wala kabila.

Amesema, β€œleo hii tunaposema mtu kwa sababu ni m-Zanzibari ndio maana amefanya mamuzi haya, kesho tusasema huyu Rais Ametoka Mbeya hana haki ya kufanya maamuzi kuhusu mgoni wa Mara. Maanake mkianza hilo jambo haliishi.”

Aidha ameongeza kuwa, “Nchi yetu ina dini na makabila lakini hayo tulikubaliana kuyaepuka kwa manufaa ya nchi yetu. Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ina pande mbili ambazo ni kitu kimoja. Viongozi wasihukumiwe kwa sababu ya tofauti zao za dini, ukabila, ukanda na rangi.”

Kwa jambo hili tutarajie maandamano - Balozi Njenga
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Juni 21, 2023