Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania ni moja ya nchi za Afrika zinazofanya mageuzi makubwa kiuchumi kwenye sera na sheria zake ili kuvutia zaidi mitaji kutoka nje ya nchi.

Rais Samia amesema hayo wakati akihutubia kwenye mkutano kati ya Wafanyabiashara wa Tanzania na India, uliofanyika jijini New Delhi ambapo katika mkutano huo, Rais Samia pia alishuhudia kubadilishana kwa hati za makubaliano baina ya Tanzania na india.

Rais Samia ameyasema hayo kwenye Kongamano la Wafanyabiashara wa Tanzania na India, lililofanyika jijini New Delhi na kudai kuwa pia Serikali imepanga kuingiza kiasi cha dola bilioni 15 za Marekani kupitia uwekezaji kutoka nje – FDI, kufikia mwishoni mwa mwaka 2025.

Aidha, Rais Samia ameongeza kuwa, India ina kila sababu ya kuwa mwekezaji namba moja Tanzania, kutokana na ushirikiano baina ya nchi hizi mbili na historia inayoziunganisha.

Ujenzi Hospitali ya Wilaya Sumbawanga watiliwa shaka
Umeme Vijijini kuboresha viwango vya Elimu - Kapinga