Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Stergomena Taxamewasili Jakarta nchini Indonesia kwa ajili ya ziara ya kikazi, ikiwa ni pamoja na kufungua rasmi Ofisi za Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini humo hapo Tarehe 22 Juni, 2023.

Dkt. Tax baada ya kuwasili Jakarta amepokelewa na Balozi wa Tanzania nchini Indonesia, Mhe. Macocha Tembele katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Soekarno-Hatta (CGK).

Akiwa nchini Indonesia, Dkt. Tax anatarajia pia kukutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Indonesia, Retno Marsudi, na kutembelea Chuo cha Diplomasia cha Indonesia.

Azam FC yakazia usajili wa Makabi Lilepo
Bahati ya mtende yamuangukia Patrick Vieira