Serikali nchini, inapanga kutumia vyanzo vyote vya asili ilivyobarikiwa ili kuzalisha umeme na kuwa na uhakika wa hitaji hilo kwa maeneo yote.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nishati, Januari Makamba kwenye maonesho ya Wiki ya Nishati Bungeni jijini Dodoma.
Kuhusu umeme wa makaa ya mawe, Makamba amesema, “tunaingiza umeme wa upepo mwakani, najua hii italeta mjadala lakini tutaingiza umeme wa makaa ya mawe mwaka 2025, na tutaingiza sasa umeme wa joto ardhi.”
Aidha, Waziri Makamba ameongeza kuwa, ‘sisi tumebarikiwa kuwa na rasilimali za asili nyingi za kuzalisha umeme na tutazitumia zote, nia ikitokea chanzo kimoja kimepata shida kingine kinaendelea.”