Serikali nchini, imesitisha usajili wa Jumuiya ya kidini ya Spirit Word Ministry iliyopo Stakishari Jijini Dar es Salaam, baada ya kubainika kutoa mahubiri na mafundisho yenye mwelekeo wa kuhamasisha vitendo vya mapenzi ya jinsia moja.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni Bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka 2023/24 na kuongeza kuwa, hatua hiyo ni mwendelezo wa kudhibiti na kupambana na vitendo vya mmomonyoko wa maadili.

Amesema, “Jumuiya hiyo imefutiwa usajili kwa sababu ya kutoa mahubiri na mafundisho yenye mwelekeo wa kuhamasisha vitendo vya mapenzi ya jinsia moja na kutoa ujumbe wenye kuhafifisha jitihada za kupambana na vitendo vya ushoga nchini.”

Masauni ameongeza kuwa, katika mwaka 2023/24 wizara imepanga kuandaa mwongozo wa taratibu za kuabudu na ithibati ya taasisi zinazotoa elimu ya dini, kuimarisha ufuatiliaji na utendaji wa Jumuiya za Kidini na zisizokuwa za Kidini.

Bola Tinubu aapishwa rasmi kuwa rais wa Nigeria
Aliyehukumiwa kimakosa aachiliwa huru baada ya miaka 33