Siku moja baada ya Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo kuagiza ujenzi wa kilometa moja ya barabara inayoenda Kituo cha Afya cha Ifingo, Mjini Mafinga Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini – TARURA, wameanza kutekeleza.

Chongolo alitoa agizo hilo baada ya kupokea malalamiko ya wananchi na ombi kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Mafinga, Cosato Chumi aliyedai ikiwa barabara hiyo itachongwa itapunguza usumbufu mkubwa
wanaokukumbana nao wananchi kuelekea kituoni hapo kupata huduma.

Kutokana na hali hiyo, Chongolo alitoa saa 24 kwa Tarura kuanza kutengeneza barabara hiyo jambo ambalo limeanza kutekelezwa, ambapo greda lilishuhudiwa likiendelea na kazi kwenye barabara hiyo muhimu kwa wananchi wanaohitaji kupata huduma kwenye kituo hicho cha Ifingo.

Chongolo yupo Mkoani Iringa kwa ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM, kuhamasisha uhai wa Chama ngazi za mashina pamoja na kusikiliza na kutatua kero za wananchi, huku maagizo mbalimbali anayotoa yakiendelea kutekelezwa.

TASAC yaelimisha jamii usafiri salama majini
Robertinho: Bado nina deni kubwa sana Simba SC