Ripoti ya Umoja wa Mataifa, imeeleza kuwa Tanzania itakuwa ya tatu kwa uchumi unaokua kwa kasi barani Afrika 2023, unaokadiriwa kufikia asilimia 5.6, na kuungana na nchi za Rwanda na Ivory coast ambayo ni mzalishaji mkubwa zaidi wa kakao duniani kwa asilimia 30.

Mageuzi kama haya pia yameleta mafanikio yanayotokana na teknolojia na uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nje wa hivi karibuni, na kupelekea ukuaji wa asilimia 7.8 wa Pato la Taifa la Rwanda kwa mwaka 2023.

Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo yenye utajiri wa madini, ambayo Mataifa washirika wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), yatasajili ukuaji wa wastani kwa mwaka 2023 takwimu ambazo zimetolewa na Umoja huo wa Mataifa uliozilenga nchi 30 zenye uchumi mkubwa zaidi barani Afrika.

Aidha, Benki ya Dunia – WB, imeiweka Tanzania katika nafasi ya 10 kwa utajiri barani Afrika kwa jumla ya pato la taifa (GDP), kulingana na kiwango cha ubadilishaji wa fedha kilichopo ikiungana na chi Ivory Coast, Ghana, Kenya, Ethiopia, Morocco na Algeria.

Hata hivyo ripoti hiyo imesema, “kwa sasa Nigeria ndiyo nchi yenye uchumi mkubwa zaidi barani Afrika ikifuatiwa na Afrika Kusini na Misri huku Tanzania ikiwa si miongoni mwa mataifa 10 ya juu kiuchumi barani humu kwa Pato la Taifa kwa kuzingatia usawa wa nguvu za ununuzi (PPP).”

Ingawa Tanzania pamoja na Cote d’Ivoire na Rwanda zitapanda kwa kasi katika ukuaji, hali itakuwa tofauti kidogo kwa bara hilo kwani ukuaji wa uchumi wa Afrika unatarajiwa kuathiriwa vibaya na sababu kadhaa mwaka 2023 na hivyo kushuka toka asilimia 4.1 iliyosajiliwa mwaka jana (2022), hadi asilimia 3.8 kwa mwaka huu (2023).

Aidha, ripoti hiyo pia imebainisha kuwa, “mauzo ya nje yataendelea kupungua na wawekezaji kuhofia kupoteza pesa zao, wakati ukuaji kwa mwaka 2023 ukitarajiwa kuongezeka kwa Afrika Magharibi, na ukitarajiwa kusalia katika hali yake ya kawaida kwa Afrika ya Mashariki na Kati.”

Kwa upande wa Kaskazini na Kusini mwa Afrika, ambao una uchumi mkubwa zaidi kutashuhudiwa kwa ushukaji wa ukuaji wa uchumi ukichangiwa na ongezeko kubwa la mfumuko wa bei duniani, gharama kubwa za ukopaji na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Aidha, imebainisha kuwa, ukuaji chanya kwa uchumi wa Kiafrika katika kipindi hicho unamaanisha kuwa kampuni kubwa zitalazimika kufanya vizuri ili zipate matokeo chanya, huku Kongo ya DRC ikitarajia kukuza uchumi wake kwa haraka mwaka huu kutokana na kuongezeka kwa uchimbaji madini, licha ya changamoto za kiusalama za eneo la mashariki mwa nchi hiyo.

“Ingawa kuna hatari kadhaa kwa kasi ya ukuaji wa uchumi wa nchi, chanya zimewekwa kuwa kubwa zaidi kuliko hasi, na kwa Uganda ambayo jumla ya Pato la Taifa mwaka 2021 lilikuwa dola bilioni 40.5, mtazamo wa kiuchumi utaendelea kuwa na changamoto,” ilisema ripoti hiyo.

Hata hivyo, nchi wanachama wa EAC zitasajili ukuaji wa wastani wa uchumi kwa 2023 kulingana na makadirio na Kenya, ambayo licha ya kuwa miongoni mwa mataifa saba yenye nguvu kiuchumi barani humo, itakuwa na mtazamo usio na uhakika wa kiuchumi.

Afrika Kusini, ambayo inachukuliwa kuwa nchi yenye uchumi ulioendelea zaidi barani Afrika ikiwa na ongezeko kubwa la asilimia 25 ya Pato la Taifa mwaka 2021, imekuwa ikikabiliana na mgogoro mkubwa kiasi cha kupelekea hali kudorora na kukosa umeme wa uhakika.

Aidha, itambulike kuwa Morocco, nchi kubwa ya kiuchumi ya eneo la Magharibi na hivi karibuni ilipongezwa na Shirika la Fedha la Kimataifa – IMF, kwa mafanikio yake ya kiuchumi ambapo hata hivyo, bila ukame, vita wala mfumuko wa bei inatarajiwa kuathiri kiwango chake cha ukuaji cha asilimia 3 ya kadirio taasisi ya Bretton Woods.

Kisa Kane, Man Utd kuifanyia umafia Spurs
Robertinho: Hatupaswi kuangalia matokeo ya Dar