Tanzania kwa miaka mitatu imetajwa kuongoza barani Afrika katika huduma za fedha jumuishi huku ikishika nafasi ya sita Duniani kwa huduma hizo licha ya kuwa 16% tu ya Watanzania wanaotumia huduma za fedha jumuishi nchini.
Takwimu hizo zimetolewa leo na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashantu Kijaji wilayani Chato Mkoani Geita wakati wa ufunguzi wa tawi la CRDB wilayani hapo, na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, JPM ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo.
Kijaji amsema kuwa mafaniko hayo makubwa yamekuja kutokana na usimamizi mzuri wa huduma za kibenki nchini.
Aidha, Naibu Waziri huyo amesema utekelezaji wa mpango wa huduma ya fedha jumuishi ya kwanza imeweza kuwafikia watanzania kutoka 58% ya hapo awali mpaka 65% ijapokuwa bado ni asilimia ndogo sana ya Watanzania wanaotumia huduma hiyo.
-
Nilishasema hakuna maandamano- JPM
-
Video: Lissu ataja sababu za kutompuuza Musiba.
-
Video: Msimamo wa Tundu Lissu akirejea nchini.
Rais alipata nafasi ya kuhutubia katika ufunguzi huo, na kuomba uongozi wa CRDB, kulegeza masharti na kupunguza riba katika mikopo ili kuwawezesha watanzania kukopa fedha kwa ajili ya kuleta maendeleo.
Aidha, Magufuli amechukua nafasi hiyo kuipongeza benki ya CRDB kwa utendaji mzuri wa kazi kwani ndiyo benki pekee Tanzania inayohudumia watu wengi kutokana na kuwekeza matawi yake katika pande zote za nchi.