Tanzania imekuwa Nchi ya Pili katika mifumo imara ya masuala ya usalama wa kimtandao (Cyber Security) Barani Afrika, huku ikishika nafasi ya 37 kidunia.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt Faustine Ndugulile leo Alhamisi (Julai 1, 2021) jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa tovuti na mpango mkakati wa wizara ya mawasiliano na teknolojia ya habari.
Ndugulile amesema serikali ipo kwenye mchakato wa kukuza na kurasimisha sera za mtandaoni ili watu waweze kufanya vizuri biashara za mtandao, akiwagusia vijana zaidi amesema kwa kufanya hivyo itasaidia hata vijana kujipatia fursa ya biashara ya mtandaoni.
“Sikuizi hakuna biashara ya frame biashara zote zinafanyika kwa njia ya mtandao vijana wanaagiza bidhaa zao kutoka nchi mbalimbali kwa njia ya mtandao na kuanza kuziuza kwenye mtandao,” Amesema Ngugulile.
Katika hali ya kuimarisha masuala ya mtandaoni, Waziri Ndugulile amesema kwa sasa serikali inakuja na sheria ya kulinda faragha na taarifa za watu, lakini pia kuwa na sheria rafiki ili vijana waweze jujiajili na kuonyesha ubunifu katika mitandao.
Amesema serikali inakenda kukuza ubunifu na kuviendeleza vipaji mbalimbali, ambapo vituo vitajengwa nchini kulea vipaji hivyo.
Matarajio ndani ya miaka 5 ni kuhakikisha Tanzania inakuwa kitovu cha ubunifu katika sekta ya TEHAMA na kuendeleza taaluma mbalimbali ambazo sasa hivi ndo zipo ndani ya dunia yetu kama vile cyber security.
Halikadhalika Waziri Ndugulile ametoa rai kwa wataalamu wa TEHAMA kujisajili ili waweze kutambulika na kuendelezwa.