Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilino ya Simba SC Haji Sunday Manara amekubali maneno yaliyosemwa na Mzee Mpili baada ya kuhojiwa na Dar24 Media jana jumatano (Juni 30) jijini Dar es salaam.

Mzee Mpili ambaye kwa sasa ameshika chati kwenye mitandao ya kijamii, kufautia uzalendo wake ndani ya Young Africans alisema hadharani namna anavyomfahamu Haji Manara kabla na baada ya kuzaliwa kwake.

Baada ya mahojiano hayo kurushwa hewani jana Jumatano jioni Haji Manara alifuatilia na kuandika kwenye ukarasa wake wa Instagram huku akimuahidi Mzee huyo wa Ikwiriri Shilingi milioni 1, endapo Young Africans itafanikiwa kuifunga Simba SC Jumamosi (JULAI 03).

“Mzee wangu Mpili amekuwa Star mkubwa nchini kwa maneno yake yenye chumvi nyingi.”

“Mimi ninamkubali sana ngendembwe zake na ninamuahidi Uto wakipata ushindi na Simba nampa milioni Cash.”

“Eti Mzee Hassan Haji alikataa mwanae asiolewe kisa yeye Simba. hahahahaha ila Story hiyo ni kweli kabisa 100%.” ameanzika manara kuwenye ukurasa wa mtandao wa kijamii wa Instagram.

Tanzania ya pili Afrika katika usalama wa kimtandao
Hitimisho la UMISSETA kesho