Tanzania imefanikiwa kupata medali ya fedha kwenye mchezo wa kurusha Mkuki  kwenye mashindano ya Afrika ya vijana yanayofanyika kwenye Uwanja wa Levy Mwanawasa, nchini Zambia.

Mwanariadha Mwanaamina Hassan Mkwayu ndiye aliyetwaa medali hiyo akirusha mkuki umbali wa meta 47.83.

Mwanaamina ametwaa medali hiyo baada ya wanariadha wengine saba wa timu ya Taifa ya riadha chini ya umri wa miaka 18 na 20 kufanikiwa kuendelea na hatua ya Nusu Fainali kwenye mashindano hayo.

Walioingia ni Mpaji Lukindo meta 400 wa U-18 akitumia sekunde 49.8 kwa wanawake meta 100 ni Nasra Abdallah akitumia sekunde 12.5 na Berther Ernest kwa sekunde 12.74.

Kwa wanaume meta 100 miaka 18 ni Alex Sezario akitumia sekunde 11.4, Said Alli sekunde 11.4, Benedicto Mathius wa U-20 alitumia sekunde 11.2 na Gasisi Geagasa wa U-20 chini alitumia sekunde 11.12.

Kwa mujibu wa kocha wa timu hiyo, Alfredo Shahanga, medali hiyo imewapa faraja baada ya wachezaji saba kufuzu Nusu Fainali.

Tutaendelea kumtunza atakuja kufanya vizuri zaidi kwenye mashindano yajayo, tunaamini tutarudi na medali zaidi ya hiyo,” amesema Shahanga Timu ya Tanzania ina wachezaji 15 wanawake na wanaume kwenye mashindano hayo ambayo yalianza Aprili 27 na yanatarajiwa kumalizika kesho Jumatano (Mei 3).

Wanahabari waaswa uzingatiaji maadili, ukweli wa taarifa
Serikali yapiga marufuku uhamisho holela