Beatrice Shellukindo, aliyekuwa Mbunge wa Kilindi mkoani Tanga, amefikwa na umauti jana akiwa hospitalini jijini Arusha.

Taarifa za msiba  huo zimethibitishwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM), kupitia Katibu wa chama hicho wilaya ya Kilindi, Hawa Nanganyau.

Nanganyau ameeleza kuwa marehemu ambaye alikuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (CCM) kutoka wilayani humo, alifariki kutokana na maradhi ya mgongo na miguu yaliyokuwa yanamsumbua kwa muda mrefu.

Mazishi yamepangwa kufanyika Jumatano, Julai 6 mwaka huu.

Dar24 imeguswa na inatoa pole kwa Taifa kwa ujumla. Apumzike kwa amani.

Lowassa ateta na Rais Kenyatta, Rutto nchini Kenya
Chadema wakusanyika Dodoma ‘kusaidia Polisi kuzuia mkutano Mkuu wa CCM’