Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene ameutaka uongozi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii, TASAF kuwashirikisha katika mchakato wa kubaini walengwa halisi ambao ni masikini, huku akiwasitiza kuwatumia Maafisa Maendeleo ya Jamii katika mchakato huo.

Ametoa kauli hiyo wakati wa ziara yake ya kikazi Jijini Dar es Salaam, ikiwa ni muendelezo wa kuzungumza na watumishi kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji na kusema licha ya TASAF kufanya kazi yake nzuri ya kukwamua kaya masikini, bado kuna minong’ono kuwa wanaopata ruzuku hiyo sio walengwa.

Waziri Simbachawene amesema, TASAF msingi wake ni mpango shirikishi wa kuondoa umasikini hivyo inatakiwa kushirikisha viongozi katika maeneo husika, ili iweze kutimiza azma ya kuanzishwa kwakwe

Amesema, TASAF bado inahitajika kwa vile bila uwepo wake umasikini ungekuwa umeongezeka kwa kiasi kikubwa na kusisitiza kuwa itaendelea kuzikwamua kaya masikini.

Naye Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma, Ridhiwani KIkwete amewapongeza wafanyakazi wa TASAF kwa kazi nzuri wanayoifanya huku akisisitiza kuwa FASAF imesaidia ongezeko la wanawake katika shughuli za kiuchumi.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Shedrack Mziray, amesema atatekeleza maagizo yote yaliyotolewa na viongozi hao ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa walengwa ndio wankuwa wanufaika namba moja.

Gara B awapa Vijana mbinu za kufanikisha ndoto
Sababu vitambulisho vya NIDA kuchelewa