Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Nchini – TAWIRI, imetakiwa kuwa na ubunifu katika utekelezaji wa majukumu yake ya Utafiti wa Wanyamapori.
Wito huo umetolewa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Angellah Kairuki wakati alipokuwa akizungumza na Menejimenti na watumishi wa TAWIRI, jijini Arusha.
Amesema, “lazima mchape kazi, muwe wabunifu na muendelee kujifunza kwa wengine na kushirikiana na taasisi zingine zinazofanya kazi zinazofanana na sisi ziwe za kitaaluma, vyuo vikuu na zinginezo.”
Aidha, amewataka kutafuta vyanzo vingine vya mapato kutoka kwa wadau mbalimbali, ili kuiinua taasisi hiyo na kutoa mapendekezo ya mazao mapya ya utalii, ili kuikuza Sekta hiyo.