Mkurugenzi wa Wakala wa Majengo nchini Mhandisi, Elius A. Mwakalinga amekiri picha zinazosambaa mitandaoni zikionyesha majengo mapya ya mabweni ya UDSM yana nyufa ni za majengo hayo, huku akisema ni kitu cha kawaida kwa majengo makubwa.
Ameyasema hayo wakati akifanya mahojiano na kituo kimoja cha redio kilichopo jijini Dar es salaam, ambapo amekiri kutokea kwa nyufa hizo, huku akisema majengo hayo yamekidhi vigezo vyote na vipimo wakati wa ujenzi wake.
“Kila design tunayofanya ya majengo sasa hivi tunatumia expansion joint, majengo mengi makubwa huwa inatumia hiyo, hivyo ni common na sio creck kubwa sana kama inavoonekana kwenye picha, nilienda ile jana usiku kukagua tukakuta hiyo hali ni process za majengo ili yaweze kuwa sawa, hivyo watu wawe na amani kabisa wala wasiwe na hofu,”amesema Mwakalinga
-
Waziri Kigwangalla afanya ziara bandarini, akamata magogo 938
-
Serikali yapanga kuajiri walimu 11,000
-
Serikali kukabiliana na nguvu za atomiki mipakani
Hata hivyo, ameongeza kuwa watu wanaosambaza picha hizo bila kutaka ufafanuzi kutoka kwake wanafanya makosa kwani wanawatia hofu watu kwa jambo la kawaida kwenye hatua za ujenzi.