Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha ameiagiza Tume ya Nguvu za Atomiki nchini, kuhakikisha inaweka vituo vya ukaguzi wa viwango vya mionzi kwa bidhaa zote zinazoingia na kutoka nchini katika mipaka yote kwa lengo la kudhibiti mionzi katika bidhaa hizo.

Ametoa agizo hilo jijini Arusha alipotembelea Tume hiyo ili kujionea jinsi inavyofanya kazi, ambapo amesema ni muhimu vituo hivyo kuwekwa katika mipaka ili kuhakikisha bidhaa zinazoingia na kutoka nchini zinakuwa na viwango vya mionzi inayokubalika kimataifa.

Ameitaka Tume hiyo kutokuishia katika kutekeleza majukumu ya kudhibiti na kuhamasisha matumizi bora ya mionzi bali inapaswa kuanza kuangalia namna bora ya kuhamasisha matumizi chanya ya nyuklia kwa maendeleo ya taifa katika nyanja za Afya, Kilimo, Maji na Teknolojia.

Magazeti ya Tanzania leo Desemba 4, 2017
Video: Tamasha la RC Makonda lafanyika jijini Dar