Timu ya Taifa ya Tanzania ya ulemavu ‘Tembo Warriors’ imefuzu kucheza Fainali Kombe la Dunia baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Cameroon mchezo uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Ushindi huo umeifanya Tembo kutinga nusu fainali na timu zote nne zinakuwa zimepata tiketi ya kushiriki fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika mwakani nchini Uturuki.
Kufautia ushindi huo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameipongeza Tembo Warriors kupitia ukurasa wake wa Instagram.
“Naipongeza Timu ya Taifa ya Walemavu ya Mpira wa Miguu (Tembo Warriors) kwa kufuzu Kombe la Dunia nchini Uturuki Oktoba, 2022.”
“Nawapongeza viongozi wa Wizara na TAFF na nawataka mfanye maandalizi mazuri zaidi kuelekea michuano hiyo ili tuwe na timu bora itakayotutangaza vyema.”