Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilino ya Mtibwa Sugar Thobias Kifaru, anaamini kikosi chao kinapitiwa wakati wa mapito na muda si mrefu kitarejea kwenye makali yake.

Mtibwa Sugar haijapata ushindi katika michezo saba ya Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu 2021/22, huku jana Jumanne (Novemba 30) ikipoteza dhidi ya Azam FC kwa kufungwa bao 1-0, Uwanja wa Azam Complex Chamazi jijini Dar es salaam.

Kifaru amesema Uongozi wa Mtibwa Sugar kwa kushirikiana na Benchi la Ufundi unaendelea kusaka mbinu mbadala ambazo wanaamini zitawarudisha kwenye mstari wa kupata matokeo mazuri.

“Tumeanza vibaya ligi, hatujafanya vizuri kwenye mechi saba tulizocheza, Nadhani tumepitiwa na upepo mbaya tu, tunaamini tutarudi katika ubora wetu. Tunarejea katika mashamba ya miwa kujipanga zaidi.” amesema Kifaru

Kufuatia mambo kuwaendelea kombo katika michezo saba iliyopita Mtibwa Sugar inaburuza mkia wa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa na alama 2.

Tembo Warriors kucheza Kombe la Dunia, Rais aipongeza
Clatous Chama amaliza utata