Taasisi ya Elimu Tanzania – TET, imepokea vifaa vya kielektroniki vya kuimarisha ufundishaji na utunzaji data, vilivyotolewa na Shirika la Shangai Edu Tech la nchini China, kwa lengo la kuimarisha ufundishaji na utunzaji data Kmkwa njia ya kielektroniki.
Vifaa hivyo, vimekabidhiwa na Kaimu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, TAMISEMI ambae pia ni Mkurugenzi Msaidizi Elimu Awali na Msingi, Suzan Nussu kwa niaba ya Katibu mkuu TAMISEMI.
Vifaa hivyo, Seti moja yenye boksi 10 vimekabishiwa Kwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania – TET, Aneth Komba na seti mbili nyingine kwa muwakilishi wa Taasisi ya Elimu ya Amali Zanzibar, Sauda Abdallah Haji.