Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania
(TET), Dkt. Aneth Komba, amewaasa wataalamu  wa masomo mbalimbali ya ufundi kutoka katika shule za Sekondari, Vyuo vya Ufundi na Vyuo Vikuu kuweka umakini katika mapitio ya vitabu vinavyotarajiwa kuanza kutumika shuleni mara baada ya uandaaji wake kukamilika.a
 
Dkt. Komba ameyasema hayo Machi 27, 2022 katika kikaokazi na watalamu hao cha mapitio ya vitabu 34 vya kiada vya masomo ya ufundi kwa shule za sekondari za ufundi kilichofanyika mjini Morogoro ambapo amesema,kuwa vitabu hivyo vinatarajiwa kumsaidia mwanafunzi wa Kitanzania katika kupata ujuzi utakaopelekea kujiari ama kujiarika hivyo wanapaswa kuifanya kazi hiyo ya mapitio kwa weledi.
 
Nina imani kazi hii ya kufanya mapitio mnaifanya kwa uangalifu mkubwa na kwa weledi ili lengo kusudiwa litimie”, Amesema Dkt Komba

Kazi ya mapitio imefanyika kuanzia tarehe 24 hadi 30 Machi 2022 Mjini Morogoro katika Chuo cha Ualimu, Mwezi Juni 2021, Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) na Taasisi ya Teknolojia Dar es salaam (DIT) ziliingia makubaliano ya uandishi wa vitabu hivyo ambavyo vitaanza kutumika shuleni hivi karibuni. 

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Machi 28, 2022
Dkt Mpango kumuwakilisha Rais Samia UAE