Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 4.6 limetokea ukanda wa Ziwa Victoria na kuyakumba maeneo ya mikoa ya jirani ikiwa ni pamoja na Geita na Shinyanga.
Gabriel Mbogoni, Mjiolojia Mwandamizi kutoka Taasisi ya Jiolojia amesema tetemeko hilo lina ukubwa wa richa 4.6.
Amesema kuwa hali hiyo imetokana na tabia za kijografia kwakuwa Tanzania imepitiwa na mkondo wa bonde la ufa.
Mbogoni ameongeza kuwa kutokana na Tanzania kupitiwa na bonde la ufa la Afrika Mashariki ikiwa na mikondo miwili, Mkondo wa Mashariki na Mkondo wa Magharibi matukio ya mateteko ya ardhi kwenye mkondo wa bonde la ufa yataendelea kushuhudiwa.
Tukio hilo limethibitishwa na Mkuu wa Mkoani Shinyanga, Anna Mringi Macha; ameeleza kuwa hakuna madhara yaliyotokea.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Geita, Mponjoli Lotson amethibitisha kutokea kwa tetemeko katika mkoa huo na kueleza kuwa halikuleta madhara.
Profesa Tibaijuka: tiba asili si uchawi ni sayansi
Kenya kufanyiwa jaribio chanjo ya Corona