Klabu ya Manchester City boda ina matumaini ya kumsajili mshambuliaji wa FC Barcelona Lionel Messi 33, itakapofika mwaka mwaka 2021, licha ya nahodha huyo wa Barca kusema kwamba anatumai siku moja kucheza soka nchini Marekani.
- Mauricio Pochettino anatarajiwa kuwasajili baadhi ya wachezaji wa Tottenham ikiwemo kiungo mshambuliaji Dele Alli, 24, na kipa wa Ufaransa Hugo Lloris, endapo kocha huyo raia wa Argentina atathibitishwa kuwa mkufunzi Paris-St Germain.
- Wolves huenda ikawasilisha ombi la kumsajili Diego Costa, 32, kuchukua mahala pake mshambuliaji wa Mexico Raul Jimenez, 29, baada ya mshambuliaji huyo wa Uhispania kukubali kusitisha kandarasi yake katika klabu ya Atletico Madrid na kuwa mchezaji huru mwezi Januari.
- Klabu ya Tottenham inataka ya kumsajili kiungo wa kati wa Austria Marcel Sabitzer, 26, mwezi Januari kulingana na klabu yake RB Leipzig.
- Klabu ya Arsenal imesitisha mpango wa kumnunua mchezaji wa Lyon na Ufaransa Houssem Aouar wakati dirisha la uhamisho la mwezi Januari litakapofunguliwa.
- Majogoo wa jiji (Liverpool) imesitisha mpango wa kumsajili beki wa kati wa Inter Milan Milan Skriniar, 25, baada ya kukasirishwa na dau la £54m lililowasilishwa na klabu hiyo ya Italia.
- Beki kutoka nchini Hispania na klabu ya Chelsea Marcos Alonso, 30, anatarajiwa kurudi Uhipania na kujiunga na Atletico Madrid kwa mkopo katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari . Alonso hajaichezea Chelsea tangu tarehe 26 Septemba.