Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua Balozi Stephen Patrick Mbundi kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki atakayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki akichukua nafasi ya Balozi Prof. Kennedy Godfrey Gastorn ambaye ameteuliwa kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Rais Samia pia amewateua Majaji wa Mahakama ya Rufani na Majaji wa Mahakama Kuu, usiku wa kuamkia leo Septemba 4, 2023 kama inavyoonekana katika taarifa iliyotolewa kwa Vyombo vya Habari na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus.

Utamaduni kuiombea Nchi uendelezwe - Dkt. Mwinyi
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Septemba 4, 2023