Dakika chache baada ya Shirikisho la Soka Tanzania kutoa taarifa za kufungiwa maisha kwa Mwenyekiti wa Klabu ya Kiteyose inayoshiriki Ligi ya Championship Yusuph Kitumbo sambamba na Kocha Mkuu wa klabu hiyo Ulimboka Mwakingwe, Shirikisho hilo limekosolewa kwa maamuzi hayo yaliyotolewa kupitia Kamati yake ya Maadili.

Kabla ya kusikilizwa kwa kesi hiyo TFF iliingizwa kwenye hisia za kutokutenda haki kutokana na Taarifa iliyothibitisha kupokelewa kwa malalamiko ya upangaji wa matokeo katika mchezo wa Ligi ya Championship kati ya Fountain Gate iliyokua nyumbani kucheza dhidi ya Kitayose yenye maskani yake mjini Tabora.

Jemedari Said Kazumari ndio mdau mkuu ambayo alionesha wasiwasi huo, na leo Ijumaa (Mei 12) amethibitisha kile ambacho alikuwa akikihisi kupitia wasiwasi wake mwishoni mwa juma lililopita.

Kama ilivyokawaida yake Jemedari ametumia Kurasa zake za Mitandao ya kijamii kueleza kile ambacho anaamini kimeibeba Kiteyose kwa kumtoa kafara kiongozi wake Yusuph Kitumbo ambaye pia ni alikuwa Mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Tabora kabla ya maamuzi ya kufungiwa hayajangazwa leo Ijumaa (Mei 12).

Jemedari ameandika: TFF YAIBEBA KITAYOSCE, YAMFUNGIA KITUMBO NA ULIMBOKA MAISHA.

TFF imeamua kuipendelea timu ya KITAYOSCE kwa kutokuidhibu kwa kashfa ambayo imethibitika ya kupanga matokeo na badala yake imemfungia maisha Mwenyekiti wa klabu hiyo Yusuph Kitumbo na Kocha Ulimboka Mwakingwe.

Yani unamtia hatiani Mwenyekiti wa klabu kwa kupanga matokeo halafu klabu yake aliyokuwa anaiwakilisha katika upangaji huo wa matokeo inasalimika. Hiki ni kichekesho cha mwaka 2023!

Swali ni kwamba Mwenyekiti alikuwa anapanga matokeo kwa niaba ya klabu gani kama sio KITAYOSCE?

Ndiyo maana hata klabu iliyolalamika iliilalamikia KITAYOSCE kurubuni wachezaji wake ili wapange matokeo.

Sasa klabu inabakije salama? Hapa napo panahitaji akili kubwa kuona kwamba watu wameamua kuipendelea timu kwa maslahi madogo madogo!

Mwaka 2016 wakati Kitumbo na wenzake wanafungiwa maisha kwenye kashfa ya kupanga matokeo na vilabu vilivyohusika pia viliadhibiwa.

Kama kilichobadilika ni kanuni basi wakati huu tuna kanuni za hovyo na ajabu sana, kama kilichobadilika ni watawala ambao wameweka maslahi binafsi mbele basi wanapaswa kujitathmini kama wanatosha kuendelea hapo walipo.

Vinginevyo kama mpira wetu unaugua basi watauacha ICU na kama uko ICU wataucha ushakufa kabisa. Hili ni moja ya mambo ya hovyo kuamuliwa kwenye uongozi huu, huwezi kumtia hatiani Mwenyekiti kwa kupanga matokeo klabu aliyokuwa anaiwakilisha ikasalimika, labda uniambie hata Kitumbo hana hatia wala hakukua na uthibitisho wa kutosha kumtia hatiani ila wamefanya kwa presha za mtandaoni.

Lakini kama uthibitisho ulitosha KITAYOSCE walistahiki adhabu kwakuwa kesho klabu zingine hata za ligi zitapanga matokeo watafungiwa Wenyeviti tu.

Shame on you guys!

BIN KAZUMARI MTIPA (The voice of the voiceless)

TETESI: Mkataba wa Beleke kuvunjwa Simba SC
Homa ya ini ni hatari kuliko HIV, kifua kikuu - WHO