Mashirika ya afya likiwemo la Afya Duniani WHO, yanaonya kuwa homa ya ini inaweza kuua watu wengi zaidi ifikapo mwaka wa 2040 kuliko HIV, kifua kikuu, na malaria kwa pamoja ikiwa ugonjwa huo utaendelea kupuuzwa na kutofadhiliwa vya kutosha.

WHO, inasema homa ya ini, inaathiri zaidi ya watu milioni 350 ulimwenguni na kuua zaidi ya watu milioni 1. Asilimia 90 ya watu wanaoambukizwa na kuuawa na ugonjwa huo ni kutoka nchi zenye pato la chini na la kati.

Aidha, licha ya tiba ya homa ya ini aina ya C na chanjo dhidi ya homa ya ini aina ya B, watetezi wa ulimwengu bado hawajafikia lengo lao ambapo gharama ya jumla ya kuponya mgonjwa ilishuka kwa asilimia 96 kutoka zaidi ya dola 2,500 kwa kila mtu hadi chini ya dola 80 kwa kila mtu aliyeponywa.

Mkurugenzi Mkuu wa Mpango wa Homa ya Ini Duniani, Oriel Fernandez anasema kwenye kituo cha Clinton Health Access Initiative au CHAI“Katika kipindi cha miaka 10 iliyopita, wameshuhudia mafanikio makubwa katika safari hii ya kutokomeza homa ya ini.

Ameongeza kuwa, “gharama ya jumla ya kuponya mgonjwa ilishuka kwa asilimia 96 kutoka zaidi ya dola 2,500 kwa kila mtu hadi chini ya dola 80 kwa kila mtu aliyeponywa.

TFF yakosolewa kumfungia Kitumbo, Mwakingwe
Muujiza: Vichanga vyakutwa vikielea juu ya maji, vyaokolewa