Tanzania na China zimeendeleza na kuimarisha ushirikiano wa Kidiplomasia, Uchumi, Afya, Elimu na masuala mbalimbali ya Kiuchumi na kubafilishana Teknolojia, ambapo kwa sasa biashara kati ya mataifa hayo imepanda thamani kutoka Dola za Kimarekani milioni 200 mwaka 2017 hadi milioni 600, huku ikitarajiwa kupanda zaidi kwa mwaka ujao 2024.

Hayo yamebainishwa na Balozi wa Tanzania nchini China anayemaliza muda wake Mbelwa Kairuki, ambaye kwa sasa amepangiwa Kituo kipya cha kazi Nchini Uingereza, wakati akifanya Mahojiano Maalum na Kituo cha Luninga cha jijini Beijing, ambacho kilitaka kupata ufafanuzi wa yale aliyofanya ndani ya miaka sita ya Ubalozi Nchini humo.

Balozi wa Tanzania nchini China anayemaliza muda wake, Mbelwa Kairuki (kushoto), katika picha na Meneja wa Dar24 Media, Abel Kilumbu, wakati wa mahojiano maalum katika Studio za Dar24, zilizopo Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Amesema, wakati wa Uviko19 Mataifa mengi yalipitia hali ngumu Kiuchumi lakini bado China iliendeleza ushirikiano wa Kiuchumi na Tanzania kwa njia zilizozingatia masharti ya Uviko19 huku akiipongeza Kampuni ya Silent Ocean ambayo ilikuwa kipaumbele katika kutafuta njia mbadala wa kusafirisha mizigo ya Wafanyabiashara wa Kitanzania.

Balozi Mbelwa Kairuki katika moja ya mahojiano aliyowahi kuyafanya na na kituo cha Televisheni cha CGTN kuzungumzia mahusiano kati ya Tanzania na China jijini Beijing, China. Picha ya Instagram.

Balozi Kairuki ameongeza kuwa, “hata sasa baada ya Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) kuongeza ratiba zake za safari na usafirishaji mizigo, imefungua milango zaidi ya kibiashara na Mahusiano na China jambo ambalo litawarahisishia Watanzania kuwa na uhakika wa kufika China moja kwa moja bila kuwa na ulazima wa kuunganisha Ndege maeneo mengine.”

Aidha, amelitumia nafasi hiyo kumshukuru Rais Dkt. Samia kwa kuendelea kumuamini, Mawaziri waliopita na wa sasa Stregomena Tax kwa ushirikiano waliompa huku akimtakia kheri Balozi mpya Khamis Mussa Omar, ambaye ameeleza kuwa ni Kiongozi mwenye weledi na uwezo mkubwa atakayendeleza na kufanya mengi katika wakati wake wa uongozi Nchini humo.

Malisa awataka Walimu kujiwekea akiba, amana
Zimbabwe: Chama tawala, Upinzani wachuana vikali