Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbas amesema mapato ya utalii yameongezeka maradufu kutoka Dola za Marekani 1.310.34 (TZS Trilioni 3.01), 2021 hadi Dola 527.77 (TZS Trilioni 5.82), baada ya ongezeko la watalii nchini lililotokana na matunda ya Royal Tour.
Dkt. Abbas ameyesema hayo jijini Dodoma wakati akielezea mafanikio ya mwaka mmoja tangu Rais Samia Suluhu Hassan alipozindua filamu ya The Royal Tour jijini Arusha na kujenga hamasa kwa watalii na wawekezaji ambayo imekuwa na manufaa kwa sekta ya usafiri wa anga baada ya kuongezeka pia kwa ruti za ndege za kimataifa uwanja wa KIA kwa asilimia 28 kutoka miruko 6,115 April 2021 hadi 7,850 April, 2023.
Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbas.
Amesema, “kutokana na watalii kuongezeka nchini ikiwa ni matunda ya Royal Tour, mapato ya jumla ya sekta hii yameongezeka kutoka Dola za Marekani 1.310.34 (Sawa na TZS Trilioni 3.01) mwaka 2021 hadi Dola za Marekani,527.77 (sawa la TZS Trilioni 5.82) imefanya Tanapa na NCAA wamevunja rekodi ya mapato.”
Aidha, Dkt. Abbas ameongeza kuwa ushiriki wa Rais katika filamu ya Royal Tour nao umeleta mafanikio ambapo Novemba 2022 huko Dallas, Texas, USA, Taasisi ya Tuzo za Afrimma ilimtangaza Rais Samia Suluhu Hassan kuwa Rais Mwanamke wa kwanza Afrika Kushinda Tuzo ya Mageuzi Katika Uongozi, wakitamka bayana kuwa mojawapo ya vigezo na mafanikio ni ushiriki wake katika Royal Tour.