Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Katiba na Sheria kuweka mfumo mzuri wa kushughulikia changamoto za kisheria zitakazoibuliwa wakati wa Kampeni katika utimilifu wake.
Majaliwa ametoa agizo hilo leo Aprili 27, 2023 wakati alipozindua kampeni ya msaada wa Kisheria ya Mama Samia Suluhu Hassan ambayo itatekelezwa kwa miaka mitatu kuanzia Machi, 2023 hadi Desemba 2025.
Amesema, “tusiache wananchi wakiwa bado hawajapata majibu ya changamoto zao. Hii itasaidia kujenga taswira nzuri kwa Serikali wala kwa mamlaka ambayo imeridhia kuwepo kwa Kampeni hii na kwa wale ambao hawawezi kumudu gharama za mawakili wa kujitegemea hakikisheni wanapata huduma za kisheria bila ya upendeleo na kwa viwango stahiki.”
Kwa upande wake Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Damas Ndumbaro amesema katika kampeni hiyo, wamepanga kutoa elimu katika maeneo ya migogoro ya Ardhi, mirathi, ndoa, sheria ya mtoto katika maeneo ya Ukatili wa kijinsia na Maadili
Amesema kampeni hiyo itatekelezwa pande zote mbili za Muungano kwa kushirikiana na wadau wote ikiwemo Ofisi ya Mashtaka, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Ustawi wa Jamii, vyuo vya elimu ya juu, CHAMA cha Wanasheria nchini – TLS, mtandao wa mashirika yanayotoa huduma ya msaada wa kisheria – TANLAP, Taasisi ya Huduma za Kisheria – LSF, LHRC, EU, UNDP, WILDAF na NMB.