Uongozi wa Klabu ya Liverpool unafikiria kuamua kuhusu hatma ya kiungo wake kutoka nchini Hispania Thiago Alcantara.

Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp amekuwa akimpigia debe hadharani Thiago, ambaye aliwasili Anfield kwa shangwe nyingi alipojiunga akitokea Bayern Munich mwaka 2020.

Hata hivyo, muda wa Thiago ndani ya Liverpool umezidi kuandamwa na majeraha na msimu uliopita alianza kwenye mechi 14 pekee za ligi.

Thiago bado hajapewa nafasi ya kucheza katika kikosi cha Liverpool msimu huu akijaribu kupata nafuu kutokana na jeraha la nyonga alilolipata mwezi Aprili, mwaka huu.

Inaelezwa kuwa Thiago aliweka wazi kwa Uongozi wa Liverpool hataki kuondoka na alitaka kujiimarisha tena katika safu mpya ya kiungo.

Mkataba wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 unaisha msimu ujao wa joto na mazungumzo yamefanyika kuhusu mustakabali wake.

Klopp ni mmoja wa wale wanaotaka kuona Thiago akiongezwa muda, lakini imefahamika kuwa kuna wengine klabuni hapo ambao hawaamini kama Mhispania huyo atapata mkataba mpya.

Samuel Eto'o akalia kuti kavu Cameroon
Daktari Simba SC afunguka ya Aubin Kramo