Beki wa kati wa Chelsea, Thiago Silva amekosoa mipango ya mmiliki wa klabu hiyo bilionea Todd Boehly baada ya timu yao kutupwa nje ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya.
Chelsea ilichapwa 2-0 na Real Madrid uwanjani Stamford Bridge usiku wa juzi Jumanne, hivyo kutolewa kwa jumla ya mabao 4-0 katika hatua hiyo ya Robo Fainali baada ya wiki iliyopita kupigwa 2-0 pia uwanjani Bernabeu.
Katika Ligi Kuu ya England Chelsea ipo nafasi ya 11 kwenye msimamo ikiwa nyuma kwa alama 10 dhidi ya Top Four inayotoa tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao na wamebakiza michezo saba tu.
Hilo linakuja huku Chelsea ikitoka kutumia Pauni 600 milioni katika usajili wa madirisha mawili yaliyopita. Tajiri Boehly, aliyenunua timu hiyo mwaka jana 2022, tayari ameshawafuta kazi makocha wawili Thomas Tuchel na Graham Potter gu aliporejea.
Na beki Silva amezungumzia hali ya mambo ilivyo huko Stamford Bridge kwa kipindi cha miezi 12 iliyopita.
Silva alisema: “Nadhani hatua ya kwanza imeshafanyika na si hatua sahihi, lakini ndo ishafanyika.
Hatuwezi kuwalaumu makocha tu kama hatuwajibiki. Ni kipindi kigumu kwa klabu, kuna mambo mengi hayafanyiwi uamuzi.
Kubadili umiliki, kuleta wachezaji wapya, kuongeza watu kwenye vyumba vya kubadilishia hilo haliendani na kikosi.