Nahodha na mshambuliaji wa zamani wa washika bunduki wa kaskazini mwa jijini London (Arsenal) Thierry Henry ametajwa kuwa mchezaji bora katika historia ya Ligi Kuu ya England.
Hiyo ni kulingana na wapenzi wa soka ambao wamekuwa wakipiga kura katika Jarida la “Mirror” juu ya mchezaji bora katika historia ya Ligi kuu ya England.
The Mirror ilitaja wachezaji 32 bora wa Ligi Kuu kwa pamoja na kuendesha mchakato wa upigaji kura kwa njia ya mtoano, mashabiki walipiga kura kuchagua wachezaji walidhani ni bora katika kila mzunguko hadi kupata mshindi wa mwisho.
Mshindi huyo akawa nyota wa zamani wa Arsenal, Thierry Henry, ambaye alimshinda Ryan Giggs katika fainali kwa zaidi ya asilimia 80 za kura.
Henry Wakati wake huko Arsenal alifunga mabao 226, na kuweka rekodi ya mfungaji bora katika historia ya klabu. Pia aliwasaidia Gunners kushinda mataji mawili ya Ligi Kuu na ndoo mbili za FA chini ya Arsene Wenger.
Nafasi Tatu za Juu:
1 – Thierry Henry.
2 – Ryan Giggs.
3 – Paul Scholes na Cristiano Ronaldo.