Nyota wa zamani wa Arsenal na FC Barcelona, Thierry Henry amesema kuwa Lionel Messi siyo mchezaji wa kawaida na hajawahi kuona mchezaji wa namna yake tangu dunia imeumbwa.

Henry amenukuliwa akielezea makubwa yanayofanywa na Leo Messi, kwa uzoefu wake kama mchezaji na ugumu uliopo na kusema siyo rahisi kufanya kama ambavyo staa huyo anafanya.

“Sijawahi kuona mchezaji wa aina ya Messi, alikuwa akitaka kufunga goli basi lazima afunge, nimeona wengi hata mimi nimefanya vingi ila huyu mtu sio wa kawaida.

“Wapo watu wanaobeza, hivi unajua ni ngumu kiasi gani kutembea na mpira, kasi, chenga, kuzunguka na mpira na namna anavyolinda mpira na bado anajua nini kinakuja mbele.

“Unajua ni ngumu kiasi gani kufanya yote haya. Binafsi huwa nashangaa anawezaje kufanya haya na hachoki,” alisema Henry

Mbaroni kwa kutupa Vichanga mapacha wa siku moja
Mazingira yaboreshwe kuvutia Wawekezaji - Kigahe