Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Rex Tillerson amepongeza hatua ya Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta na mpinzani wake Raila Odinga ya kukutana na kumaliza tofauti zao za kisiasa.

Rais Uhuru Kenyatta na mpinzani wake mkuu wa kisiasa, Raila Odinga wametangaza kuanzisha juhudi za kuliunganisha taifa hilo ambalo lilikuwa limegawanyika kwa misingi ya kikabila.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Nairobi, Tillerson amesema kuwa alizungumza na viongozi hao juu ya hatari zinazoikabiri nchi hiyo kimataifa.

Hata hivyo, Tillerson yuko kwenye ziara ya wiki moja barani Afrika ambapo tayari amezitembelea nchi za Ethiopia, Djibouti na Kenya na anatarajiwa kuondoka Nairobi siku ya Jumatatu kuelekea Nigeria na Chad.

Maandamano yanayohamasishwa na Mange Kimambi ni uhaini
Video: Watakao andamana watasimulia- JPM, Maandamano ya Mange Kimambi yaleta hofu mpya