Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoani Njombe imewahukumu kunyongwa hadi kufa Washtakiwa tisa akiwemo Beatus Salum aliyekuwa Mtendaji wa Kijiji cha Kipengere Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe kwa makosa ya mauaji ya Ndugu wawili.
Kesi hiyo ya mauaji namba 11 imetolewa hukumu na Hakimu wa Mahakama hiyo, Zabibu Mpangule mbele ya Washtakiwa, Mawakili wa utetezi na Mwendesha mashtaka kwa makosa ya mauaji ya Watu wawili, Francis Chaula na Fabio Chaula.
Amemesema, April 27, 2020 katika Kijiji cha Kipengere Washatkiwa wote waliwaua ndugu hao ambao ni mtu na kaka yake na taarifa za uchunguzi wa miili hiyo iliyotolewa na Daktari ilisema sababu vifo ni uvujaji wa damu nyingi uliosababishwa kupigwa na vitu vizito.
Aidha, Hakimu Mpangule ameongeza kuwa mshtakiwa namba 6,7,8 na 9 ambao walikuwa ni Viongozi akiwemo Mwenyekiti wa Kijiji, Mtendaji wa Kijiji pamoja na Mwenyekiti wa CCM wa Tawi, wanaingia katika hukumu hiyo kutokana na kufanya vikao vilivyokuwa vikihusu mauaji kama ilivyoelezwa na mshtakiwa namba 5 kwenye kesi hiyo kumuua Frank Chaula kulipa kisasi wakidai amekuwa akiwasumbua.