Meneja wa Mamlaka ya hali ya hewa mkoa wa Manyara Selva Mziho, amesema kuwa mvua katika mkoa wa Manyara zitakuwa chini ya wastani hadi wastani hivyo hazitokuwa na madhara yoyote kwa wananchi mkoani hapo.
Selva ametoa taarifa hiyo kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha katika baadhi ya maeneo nchini na kusema kuwa mvua hizo zitadumu ndani ya miezi miwili kuanzia Novemba 2020 hadi Januari 2021.
Selva amewataka wakulima mkoani hapo kuanza kuandaa mashamba na kufuata ushauri unaotolewa na afisa ugani juu ya kilimo kutokana na hali ya mvua.
Aidha, amesema kama mvua itabadilika na kuwa kubwa katika mkoa huo, haitokuwa na madhara lakini ni vyema wananchi kuchukua tahadhari mapema, hasa kwa wale waishio mabondeni.