Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania (TMA), imetoa angalizo la kuwepo kwa mvua kubwa kwa baadhi ya maeneo ya ukanda wa pwani ya Bahari ya Hindi kwa siku mbili.
Maeneo ambayo yanatarajiwa kukumbwa na mvua hiyo ni mikoa ya Tanga, Dar es salaam, Pwani, kaskazini mwa Morogoro na visiwa vya Unguja na Pemba.
Taarifa hiyo imetolewa leo na imesisitiza kuwa mvua hizo zitaanza Oktoba 16 hadi 17 mwaka huu hivyo wakazi wa mikoa tajwa wanashauriwa kuchukua tahadhari.
Aidha athari zinazotarajiwa kutokea ni baadhi ya makazi kuzungukwa na maji, ucheleweshwaji wa usafiri, na kusimama kwa muda kwa baadhi ya shughuli za kiuchumi na kijamii.