Serikali kupitia Shirika la Reli nchini imezindua Treni yenye mabehewa 20 itakayofanya safari zake katika nchi za Afrika Mashariki.
Hayo yamesemwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TRL, Shaban Kiko alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, amesema kuwa Treni hiyo imeanza kupeleka mizigo nchi ya Burundi huku wakisubiri utaratibu wa kuanzisha safari katika nchi zingine.
“Treni hii inayoanza safari zake itakua inachukua mizigo kutoka katika Bandari ya Dar es salaam na kusafirisha katika nchi za Afrika Mashariki,”amesema Kiko.
Aidha, amesema kuwa Shirika hilo limepunguza gharama za usafirishaji mizigo ya kawaida na ile inayohifadhiwa kwenye makasha.
Hata hivyo, ameongeza kuwa wametoa dola 3,056 kwa behewa moja la mizigo ya kawaida na na dola 3024 kwa mizigo iliyofungwa kwenye makasha.