Kiungo wa klabu ya Simba SC Clatous Chotta Chama ametemwa kwenye kikosi cha Zambia ‘Chipolopolo’ kilichotajwa juma hili tayari kwa michezo ya kuwania kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika ‘AFCON 2023’ itakayorindima mwezi ujao.
Zambia itaanza kampeni ya kusaka safari ya kufuzu Fainali za AFCON 2023, kwa kucheza dhidi ya Ivory Coast ugenini Juni 03, huku mchezo wa mzunguuko wa pili itacheza nyumbani dhidi ya Lesotho Juni 09.
Sababu kutoka Chama cha soka nchini Zambia zimeelza kuwa, Chama ametemwa kikosini, kufuatia majeraha ya kifundo cha mguu yanayomkabili katika kipindi hiki, ambayo pia yamemnyima nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha Simba SC katika michezo kadhaa ya Ligi Kuu Tanzania Bara.
Hata hivyo Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Zambia Aljosa Asanovic, amemuita kiungo Rally Bwalya kwenye kikosi chake, baada ya kumuacha kwenye kikosi kilichoitwa kwa ajili ya michezo ya kirafiki ambapo Chipolopolo ilicheza mwezi Machi dhidi ya Iraq, Congo na Benin.
Katika michezo ya kuwania kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika ‘AFCON 2023’ Zambia imepangwa Kundi H na Ivory Coast, Lesotho pamoja na Visiwa vya Comoro.
Kikosi cha Zambia kilichotajwa na Kocha Aljosa Asanovic, kwa michezo miwili ya Kundi H upande wa Walinda Lango ni Toaster Nsabata (Sekhukhune-RSA), Charles Kalumba (Red Arrows), and Cyril Chibwe (Unattached).
Mabeki: Frankie Musonda (Raith Rovers-Scotland), Tandi Mwape (TP Mazembe-DRC), Miguel Chaiwa (Athletico), Dominic Chanda (Kabwe Warriors), Benedict Chepeshi (Red Arrows), and Shemmy Mayembe (Zesco United).
Viungo: Roderick Kabwe (Sekhukhune-RSA), Enock Mwepu (Brighton-England), Emmanuel Banda (Djurgardens-Sweden), Kings Kangwa (Arsenal Tula-Russia), Rally Bwalya (Simba SC-Tanzania), Prince Mumba (Kabwe Warriors), Lubambo Musonda (AC Horsens-Denmark), Kelvin Kampamba, Spencer Sautu, (both Zesco United), Lameck Banda (Maccabi Petah Tikva-Israel), and Edward Chilufya (Midtjylland-Denmark).
Washambuliaji: Fashion Sakala (Rangers-Scotland), Evans Kangwa (Arsenal Tula-Russia), Ricky Banda (Red Arrows), Gamphani Lungu (SuperSport United-RSA Patson Daka and (Leicester City-England).