Rais wa Marekani, Donald Trump amemtaka Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan kusitisha mara moja operesheni ya kijeshi katika eneo la Kikurdi la Afrin nchini Syria.
Trump amemtaka rais Tayyip Erdogan kupunguza operesheni ya kijeshi inayofanywa na nchi yake katika eneo hilo ili kuepusha vifo vya raia.
Aidha, katika taarifa iliyotolewa na Ikulu ya White House imesema kuwa Trump pia amemuonya Erdogan kuhusu matamshi ambayo amekuwa akiyatoa kuhusu Marekani kuwa ni ya uongo na kizushi.
Kwa upande wa maafisa wa Uturuki wamepinga taarifa iliyotolewa na White House wakisema kuwa haikusema ukweli wa kile kilichozungumzwa na marais hao wawili, pia wamesema Trump hakuzungumzia kuhusu wasiwasi wa kuongezeka kwa machafuko kutokana na operesheni hiyo ya Uturuki.
Hata hivyo, wamesema kuwa wakati wa mazungumzo hayo ya simu, Rais Trump aliihakikishia Uturuki kuwa Marekani haitawapa tena silaha wapiganaji wa Kikurdi nchini Syria.
-
Trump kuhutubia kongamano la uchumi duniani
-
Rais Kagame kuteta na Trump kuhusu Afrika
-
Daktari atupwa jela maisha